Liverpool imebanwa mbavu kwenye mchezo wa derby ya merseyside dhidi ya Everton mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huu ulikua wa kasi huku vilabu vyote vikishambuliana kwa vipindi na kutengeneza nafasi ambazo zingeweza kuzaaa mabao lakini milango ilikua migumu kwa pande zote mbili huku makipa wa timu zote wakifanya kazi ya ziada kuokoa michomo iliyokua inaelekea langoni kwao.
Liverpool wanavuna alama tisa kwenye michezo sita ya ligi kuu ya Uingereza waliyoicheza msimu huu ikiwa ni rekodi mbovu kwa klabu hiyo kwa miaka ya karibuni huku wakiendelea kujiweka kwenye mazingira magumu ya kutafuta ubingwa huo mapema dhidi ya hasimu wao klabu ya Manchester City.
Huku klabu ya Everton wao wakiwa kwenye hali mbaya zaidi wakiwa wamevuna alama nne kwenye michezo sita waliyocheza mpaka ikiwa ni ishara mbaya kwa klabu hiyo baada ya kunusurika kushuka daraja msimu uliomalizika.
Liverpool wao wanapitia wakati mgumu baadhi ya wachezaji wake muhimu wakiandamwa na majeruhi wachezaji kama Thiago alcantara,Karim konate,Naby keita,pamoja na Joel Matip wachezaji hao wanasababisha klabu hiyo kupitia wakati mgumu zaidi.

