Soyuncu ameachwa na kikosi cha Leicester City ambacho kinacheza dhidi ya Brighton ugenini hii leo. mchezaji huyo ambaye anacheza katika nafasi ya beki katika klabu yake anasubiri kupewa mkataba mpya na timu yake hiyo.

Mazungumzo kati ya beki huyo na timu yake yataendelea wiki ijayo endapo ataendelea kuitumikia klabu hiyo au laah, ambapo timu yake hiyo imekuwa ikipitia wakati mgumu msimu huu kwani hawajashinda mechi hata moja toka kuanza kwa Epl.
Soyuncu amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake hasa katika nafasi ya ulinzi msimu uliopita ambapo kwa kama klabu yake itamumpa kandarasi watakuwa wameongeza kitu kutokana na kuondokewa na wachezaji ikiwemo katika nafasi ya beki.


