Klabu Sevilla ya nchini Hispania ambayo imemtimua kocha wake Julien Lopetagui imepanga kumpa kazi kocha wa zamani wa klabu ya Marseille Jorge Sampaoli kama kocha wake wake mpya.
Klabu ya Sevilla ambayo ilipoteza mchezo wake jana usiku wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya Dortmund katika dimba lao la nyumbani Ramon Sanchez Pizjuan kwa jumla ya mabao manne kwa moja ikiwa ni muendelezo wa matokeo mabaya wa klabu hiyo katika kundi hilo ambapo klabu hiyo imeambulia alama moja baada ya kupoteza michezo miwili na kusuluhu mchezo mmoja.
Kufuatia matokeo hayo mabaya ya klabu ndio yalipelekea klabu kumfukuza kazi kocha wake Lopetegui mara baada ya mchezo wa jana na klabu hiyo ikaanza kufanya utaratibu wa kumpata kocha mpya na ndipo jina la Jorge Sampaoli lilipokua juu na kutajwa kama mrithi wa Lopetagui.
Jorge Sampaoli ambaye ameshawahi kufundisha klabu ya Sevilla miaka ya 2016/17 kabala ya kwenda kujiunga na timu ya taifa ya Argentina kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi 2018 hivo kocha huyo kama atafanikiwa kutangazwa ndani ya klabu hiyo itakua ni kama amerudi nyumbani kwani ameshawahi kuhudumu klabuni hapo.

