Thiago Silva(38) Juu ya Potter

Beki wa kati wa Chelsea Thiago Silva amemuongelea kocha wao mpya Graham Potter  huku akisema kuwa kocha huyo ni mtu maalumu, mtu mzuri na pia ni mnyenyekevu sana kwa watu wote.

 

Thiago Silva(38) Juu ya Potter

Thiago anasema kuwa kocha juyo hahitaji kuwa mkamilifu dimbani, na anajua kuwasimamia vizuri wachezaji na anapata kupanga timu yake vizuri kwa mawasiliano yake ya kibinadamu na ya unyenyekevu.

Ikumbukwe kuwa Potter amejiunga na Chelsea kutoka Brighton siku si nyingi na kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tuchel baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha licha ya kufanya usajili ambao kocha alipendekeza.

 

Thiago Silva(38) Juu ya Potter

Potter mpaka sasa amecheza mechi tatu tuu akiwa na Chelsea ambapo ndani ya hizo mechi, moja ni ya ligi ambayo kashinda na zingine ni za ligi ya mabingwa, moja kashinda nyingine katoa sare.

Kocha huyo anatarajiwa kufanya mengi makubwa ndani ya klabu hiyo huku Chelsea wakianza taratibu kufatilia masuala ya usajili la Januari.

Kesho Thiago na wenzake watakuwa uwanjani kuwaalika Wolveshampton ambao siku si nyingi wamemtimua kocha wao. Msimu uliopita hakuna aliyekuwa mbabe kati yao. Je na kesho kutakuwa hakuna mbabe?.

Thiago Silva(38) Juu ya Potter

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.