Beki wa kati wa Chelsea Thiago Silva amemuongelea kocha wao mpya Graham Potter huku akisema kuwa kocha huyo ni mtu maalumu, mtu mzuri na pia ni mnyenyekevu sana kwa watu wote.

Thiago anasema kuwa kocha juyo hahitaji kuwa mkamilifu dimbani, na anajua kuwasimamia vizuri wachezaji na anapata kupanga timu yake vizuri kwa mawasiliano yake ya kibinadamu na ya unyenyekevu.
Ikumbukwe kuwa Potter amejiunga na Chelsea kutoka Brighton siku si nyingi na kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tuchel baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha licha ya kufanya usajili ambao kocha alipendekeza.

Potter mpaka sasa amecheza mechi tatu tuu akiwa na Chelsea ambapo ndani ya hizo mechi, moja ni ya ligi ambayo kashinda na zingine ni za ligi ya mabingwa, moja kashinda nyingine katoa sare.
Kocha huyo anatarajiwa kufanya mengi makubwa ndani ya klabu hiyo huku Chelsea wakianza taratibu kufatilia masuala ya usajili la Januari.
Kesho Thiago na wenzake watakuwa uwanjani kuwaalika Wolveshampton ambao siku si nyingi wamemtimua kocha wao. Msimu uliopita hakuna aliyekuwa mbabe kati yao. Je na kesho kutakuwa hakuna mbabe?.


