Klabu ya Real Madrid sasa wanakaribia kufikia makubaliano na mshambuliaji wao Karim Benzema kuongeza mkataba kwa msimu mmoja zaidi hivi karibuni.

Huku mkataba wake mpya wa mchezaji huyo na Real Madrid ukichukuliwa kama suala la wakati kwa pande zote mbili na kuwa wote wanataka kuusaini siku si nyingi na mchezaji huyo ambaye anapigiwa chapuo la kuchukua Ballon d’Or.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Kifaransa utakuwa halali hadi mnamo Juni 2024 kwani mshambuliaji huyo ataongeza mkataba na Madrid kwa msimu mmoja zaidi.

Rais wa klabu hiyo Fiorentina Perez, kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti na bodi ya klabu hiyo wako kwenye ukurasa mmoja kwani Benzema ni mchezaji muhimu kwao mwaka ujao na gwiji wa klabu hiyo.

