Thomas Muller mshambuliaji mwandamizi wa klabu ya Fc Bayern Munich ataukosa mchezo wa kesho kati ya klabu yake dhidi ya klabu ya Borussia Dortmund maarufu kama De Klassiker.
Thomas Muller ambaye alipimwa siku kadhaa nyuma na kugundulika na maambukizi ya Covid 19 hivo ataendelea kuwepo nje akiendelea kujiuguza na kupelekea kuukosa mchezo huo mkali na wenye ushindani baina ya vilabu hivo pendwa nchini Ujerumani.
Thomas Muller na Joshua Kimmich waliukosa mchezo wa katikati ya wiki wa ligi ya mabingwa barani ulaya waliposhinda mchezo huo kwa mabao matano kwa bila dhidi Victoria Plzen na watu wote hao walikua wamejitenga kwasababu ya tatizo hilo.
Joshua Kimmich yeye anatarajiwa kurudi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Borussia Dortmund baada ya kupona ugonjwa wa Covid 19 aliokua akikabiliwa nao pamoja na mchezaji mwenzake Thomas Muller ambaye anaonesha bado ana viashiria vya ugonjwa huo.
Kocha wa klabu ya Bayern Munich Julien Nagelsman amefunguka kua kiungo wake Kimmich anaendelea vizuri na hana dalili zozote tena zinaoonesha ana ugonjwa huo hivo kesho ana uwezekano mkubwa wa kua dimbani dhidi ya Dortmund.

