Beki wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Uholanzi Nathan Ake amefunguka kua ana furaha ndani ya klabu hiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza.
Beki huyo ambae alikaribia kujiunga na klabu yake ya zamani ya Chelsea katika dirisha la joto lililopita na kwasasa ameeleza kufurahishwa kubaki klabuni hapo.
Nathan Ake licha ya maneno mengi yanayoendelea kua beki huyo hawezi kupata nafasi kwenye kikosi kutokana na uwezo wake kua wa kawaida lakini beki huyo amesisitiza anahitaji kupambana klabuni hapo hata kwenye suala la kugombea nafasi yuko tayari kupambania nafasi yake klabuni hapo.
“Nina furaha nikiwa hapa City,Na nina furaha kubaki hapa kipindi hichi. Sihofii kuhusu suala la ushindani wa nafasi”Alisema Nathan Ake Alisema.Beki anatarajiwa kubaki klabuni hapo akiwa kwenye mipango ya klabu hiyo .
Manchester City wana mipango na mchezaji huyo licha ya tetesi kusema mchezaji huyo alipanga kutimka Januari kwenye dirisha dogo baada ya usajili wake kuelekea Chelsea kushindikana majira ya joto.

