Uefa Kurejea Tena Leo,Viwanja Tofauti Kuwaka Moto.

Uefa  kurejea tena leo na mechi kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti kuwaka moto leo huku mechi kati ya Ac Milan dhidi ya Chelsea ikitolewa macho zaidi.

Baada ya wiki iliyopita klabu ya Chelsea kuibamiza klabu ya Ac Milan wakiwa katika dimba lao la nyumbani kwa jumla ya mabao matatu kwa bila leo klabu hiyo itakaribshwa katika dimba la San Siro kumenyana tena na Ac Milan ambao watahitaji kulipa kisasi baada ya kujeruhiwa wiki iliyopita.uefaKlabu ya Borussia Dortmund leo watakua dimbani katika dimba lao Signal Iduna Park kuwakaribisha klabu ya Sevilla baada ya kuichabanga klabu hiyo mabao manne kwa moja nyumbani kwao wiki iliyoisha na kupelekea kumfukuza kocha wao Julien Lopetagui leo wana mlima wakupanda wakiwa ugenini katika mchezo huo.

Real Madrid nao leo watakua uwanjani nchini leo nchini Ukraine kupambana na Shaktar Donetsk ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kushinda michezo yake mitatu ya kwanza.

Paris Saint German ambao wamesuluhu michezo miwili mfululizo kwenye mchezo wa kwanza wa Uefa dhidi ya Benfica walipata sare ugenini wiki iliyopita kabla ya kusuluhu katika mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa wikiendi iliyoisha leo wana kazi wakiwa nyumbani kupata alama tatu dhidi ya Benfica walio kwenye kiwango bora kabisa kwasasa.uefaMichuano ya Uefa Champions league leo itapigwa michezo mingi lakini kuna mechi ambazo zinatolewa macho sana ni kati ya Ac Milan dhidi ya Chelsea Borussia Dortmund Vs Sevilla na PSG Vs Benfica.

Acha ujumbe