Diego simeone: Bado niponipo Atletico.

Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amedai hana mpango wa kuondoka klabuni hapo baada ya kuanza vibaya msimu huu.

Diego Simeone ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Club Brugge wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Wanda Metropolitano.diego simeoneKocha huyo alietumikia klabu hiyo kwa miaka kumi sasa akifanikiwa kubeba mataji mawili ya ligi kuu Hispania La liga na fainali mbili za ligi ya mabingwa ulaya ameeleza matumaini yake ya kubaki klabuni hapo huku wengi wakiona mda wa kuondoka umefika baada ya matokeo mabaya ambayo klabu hiyo imekua ikiyapata huku yeye akisistiza kupanda na kushuka kupo kwenye kazi hivo haimsumbui.

“Siendi Popote, Nipo hapa, Ninahisi nina usalama sawa na siku zote. Niliwahi kuulizwa kama najiona pengine jibu langu hapana kabisa” Alisema Diego simeone.diego simeoneKocha huyo atakua na kibarua leo baada ya kufungwa na Brugge mechi iliyopita na leo wako nyumbani na wanahitaji kushinda kwani mpaka sasa timu ya Simeone inashika mkia ikiwa imekusanya alama tatu pekee kwenye mechi tatu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.