Man City Yakwea kileleni Kwenye Msimamo Uingereza.

Klabu ya Man City imekwea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga klabu ya Leceater bao moja kwa bila. Mechi hiyo imeoigwa katika dimba Kingpower stadium mapema mchana wa leo na kushuhudia vijana wa Pep Guardiola wakienda kileleni mwa msimamo.

Katika mchezo huo ambao klabu ya Leicester City walionesha kutoa upinzani mkali, Lakini Man City waliokua bora zaidi na kupata matokeo chanya katika mchezo huo wa 12 kwa timu hiyo kutoka katika jiji la Manchester.man cityAlikua Kevin de Bruyne aliwalaza Leicester na viatu mapema kipindi cha pili alipopiga mkwaju mkali wa mpira wa adhabu na kuukwamisha wavuni, ambapo lilibakia mpaka mwisho wa mchezo na City kuondoka na alama tatu.

Mchezo huo ambao ulishuhudia kukosekana kwa mshambuliaji hatari wa klabu ya City Earling Haaland. Lakini haikufanya vijana wa Guardiola kushindwa kutoa adhabu kwa Leicester na kuondoka vifua mbele katika dimba la Kingpower.man cityMan City sasa wanakaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 29 huku klabu ya Arsenal wakiwa na alama 28 wakishika nafasi ya pili huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.