Mshambualia wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar amemuunga mkono nyota mwenzake wa kimataifa wa Brazil Antony. Na hii baada ya nyota huyo kushambuliwa vikali kutokana na aina yake ya kuchezea mpira.antonyMchezaji huyo ambae amesajiliwa na klabu ya Manchester united ameibua gumzo miongoni mwa wachambuzi mbalimbali kutokana na aina yake ya uchezaji. Ikiwemo magwiji wa zamani wa klabu hiyo ambao wamekua wakipinga vikali aina ya uchezaji wa winga huyo kwa kudai haina msaada na timu.

Lakini staa mwezake wa timu ya taifa ya Brazil Neymar amemuunga mkono mchezajii huyo na kumtaka asiache aina yake ya uchezaji kwani ndo imekua utambulisho wa sanaa yao kama Wabrazil. Staa huyo wa klabu ya PSG alitumia mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kutuma ujumbe wa kumuunga mkono Antony baada ya kupokea mashambulizi makali kutoka kwa wachambuzi ikiwemo Gwiji wa klabu hiyo Paul Scholes.antonyWakati huohuo Antony nae alitumia mtandao wake wa kijamii kueleza kua hatoacha aina yake ya uchezaji kwani ndo iliomfikisha hapo alipo na watu kumtambua. Vilevile ni utamaduni kwao Wabrazil kuchezea mpira kwakua kwao mpira ni burudani.

 

Miongoni mwa wachezaji waliowhi kupokea pingamizi kutokana na aina yake ya uchezaji ni Neymar na ndio maana ametoka hadharani kumtetea mchezaji mwenzake wa kibrazil. Wachambuzi wengi haswa kutoka Uingereza wamekua hawafurahishwi na aina ya uchezaji wa Wabrazil na kuona kama wanacheza mpira wa majukwaa ambao hausaidii timu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa