Manchester City wamefanikiwa kushinda mchezo wao wa tano wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu wakiwa katimba dimba Molineux stadium nyumbani kwa klabu ya Wolveshampton.

Mchezo huo ambao ulipigwa mapema kabisa kwenye muda wa saa nane mchana kwa saa za Afrika mashariki Jack Grealish aliefungua njia kwa klabu ya City baada ya kuipatia bao timu hiyo mnamo dakika ya kwanza tu ya mchezo kabla Earling Haaland kuongeza bao la pili na klabu hiyo kuongoza kwa mabao mawili mbele huku dakika ya 33 ya mchezo beki wa kati wa Wolves anapewa kadi nyekundu baada ya rafu mbaya kwa mchezaji Jack Grealish na kuwafanya Mbweha hao kucheza pungufu mpaka mwisho wa mchezo.

man cityMchezo ulionekana wa kushambuliana kwa vipindi na kipindi cha kwanza Wolves walionekana kutawala mchezo licha ya kuruhusu mabao mawili ya mapema, hali ilendelea kua sio nzuri kwa Wlves waliopo nyumbani kwenye kupindi cha pili baada ya kuruhusu bao la tatu katika mchezo huo liliofungwa na Phil Foden.

Earling Haaland anaendelea makali yake na kufunga kwa namna anavyojiskia baada ya kufunga katika mchezo ametimiza magoli 11 katika mechi 7 za ligi kuu ya Uingereza kwa mshambuliaji huyo hatari.

Manchester City wanakwea kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha alama 17 mbele ya Arsenal wenye alama 15 katika nafasi ya pili huku wakiwa hawajacheza mchezo wao wa saba wa ligi hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa