Mshambuliaji wa Real Madrid Vinicious Junior amesisitiza kuwa “hataacha kucheza” baada ya kuwa na maoni yenye dhana ya ubaguzi wa rangi kutoka kwa wakala wa soka wa Uhispania Pedro Bravo.

 

Vinicious: "Sitaacha Kudansi"

Bravo alitoa maoni yake kuhusu ushangiliaji wa goli la Vinicious wiki hii, Akiiambia El Chiringuito : “Lazima uwaheshimu wapinzani wako unapofunga bao, ukitaka kucheza Samba unapaswa kwenda kwa (Sambadrome) huko Brazili. Waheshimu wenzako na acha kucheza kitumbili”

Matamshi hayo yalileta ukosoaji mkubwa, huku wachezaji wenzake wa Kimataifa wa Brazil Neymar na Bruno Guimaraes wakiwa upande wa Vinicious huku wakisema Bravo anapaswa  ‘kufungwa jela”.

Mshambuliaji maarufu Pele pia alikashifu maoni ya Bravo, akiandika kwenye Instagram: “Kandanda ni furaha. Ni dansi. Ni zaidi ya hiyo. Ni sherehe ya kweli.

Vinicious: "Sitaacha Kudansi"

 

“Ingawa,  kwa bahati mbaya, ubaguzi wa rangi bado upo, hatutaruhusu hilo lituzuie kuendelea kutabasamu. Na tutaendelea kupambana na ubaguzi wa rangi kila siku kwa njia hii: Kupigania kwa haki yetu ya kuwa nafuraha na kuheshimiwa.”

Bravo baadae aliomba msamaha kwenye Twitter akisema kuwa “alitumia vibaya” neno hilo.

Vinicious sasa amezungumza mwenyewe juu ya taarifa hiyo, akisema katika video iliyowekwa kwenye Instagram yake : Maadamu rangi ya ngozi ni muhimu zaidi kuliko mwangaza wa macho, kutakuwa na vita. “Wanasema kuwa furaha inasumbua. Furaha ya Mbrazil mweusi aliyeshinda Ulaya inasumbua zaidi. Lakini hamu yangu ya kushinda, tabasamu langu la kung’aa machoni mwangu ni kubwa kuliko hiyo”.

 

Vinicious: "Sitaacha Kudansi"

Aliendelea kusema kuwa alikuwa ni mwathirika wa chuki dhidi ya wageni na ubaguzi wa rangi kwa kauli moja. Ni ngoma za kusherehekea tofauti za kitamaduni za Ulimwengu. Kubali. Kuheshimu. Sitaacha

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa