Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar amepanga kutindika daruga kuchezea timu ya taifa hilo baada ya michuano ya kombe la dunia ambayo yanafanyika mwaka huu nchini Qatar.

Mshambuliaji huyo anayekipiga kwenye klabu ya PSG na mfungaji bora wa Brazil, ambaye anashika nafasi ya pili kwenye taifa hilo, anatarajia kukabidhi jersey ya taifa hilo kwa mchezaji mwenzie ambaye ametoa siri hii Rodrygo.

Neymar

Neymar amepanga kumwachia Rodrygo jersey namba 10 ambyo imevaliwa na nyota wakubwa wa taifa hilo wakiwemo Pelé, Ronaldinho na Kaká. Rodrygo wakati akihojiwa na kituo cha habari cha ESPN alisema, “Neymar aliniambia, naachana na timu ya taifa na jersey namba 10 ni yako.

“sikujua hata ni mjibu nini! Niliaona aibu, nikajichekesha na hata sikuweza kumjibu ipasavyo. Nikamwambia inabidi ucheze kwa muda zaidi, kwa sasa sihitaji. alinitazama kisha akacheka.”


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa