Mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar amefunga magoli mawili kwenye mchezo ambao timu hiyo ilipoifunga timu ya taifa ya Korea ya kusini goli 5-1 jijini Seoul siku ya alhamisi, ambapo magoli yote ameyafunga kwa mikwaju ya penati.

Neymar alifanikiwa kufunga magoli yake ya 72 na 73 kwa nchi yake lakini pia akiikaribia rekodi ya nguli wa soka Duniani Peleambaye anashikilia rekodi ya kufunga magoli 77 kwa nchi yake ya Brazili katika kipindi chote alichofanikiwa kuichezea Brazili

Neymar.

Neymar kulikuwa na hati hati ya kutokuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kupata majeraha ya mguu wake wa kulia  akiwa kwenye mazoezi ya kujianda na mchezo huo siiku ya jumatano, lakini alifanikiwa kucheza na kuwa nyota wa mchezo huo akiwa na Richarlison, Philippe Coutinho na Gabriel Jesus ambapo kila mmoja alifanikiwa kufunga.

Brazili inashika namba moja kwenye viwango vya FIFA kwa ubora duniani, ambapo walikuwa bora na hatari zaidi na kupata goli la kuongoza mapema zaidi kwa kupitia goli safi la kichwa kwa Thiago Silva.

Goli pekee la kuongoza la Korea Kusini lilifungwa na mshambuliaji wa Bordeaux Hwang Ui-jo, huku mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza Son Heung-min akiambulia patupu na kushindwa kuisaidia timu yake ya taifa.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa