Mahambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette amekubaliana na klabu ya Lyon ya kurejea kwenye klabu hiyo baada ya mkataba wake kuisha na klabu yake ya sasa  ambapo kwa sasa yupo kwenye mwezi wake wa mwisho wa mkataba wake.

Klabu ya Lyon haijawai kuficha nia yao ya kutaka kumrudisha Alexandre Lacazette, ambaye ametokea kwenye akademi ya klabu hiyo, na alifanikiwa kufunga magoli 129 kwenye michezo 275 kabla ya kujiunga na klabu ya Arsenal kwa rekodi ya usajiri wenye thamani £46.5milioni mwaka 2017.

Alexandre Lacazette

“Tutafanya kila liwezekanalo ili kumsajiri tena Lacazette,” raisi wa klabu ya Lyon Jean-Michel Aulas alikiri mwezi February, na sasa wamethibitisha kuwa mazungumzo waliyoyafanya wamekubalian na wanasubili kumalizia tu.

Lacazette anaelewa kuwa tayari wameshakkubaliana masharti ya kurudi kwenye klabu yake ya utotoni, na ni maswala kidogo tu yamebaki kabla ya kufunga huu usajiri wake.

Alexandre Lacazette wakati anaelekea kumalizia mwezi wake wa mwisho kwenye klabu ya Arsenal, anaacha rekodi ya kufunga magoli 70 na kusaidia kupatikana magoli 30 kwenye michezo 206.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa