Mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal William Gallas amemkosoa Mikel Arteta jinsi anavyowatendea wachezaji wake wa timu hiyo Alexandre Lacazette na William Saliba, alipoulizwa kama anaona wachezaji hao wataendelea kubaki kwenye timu hiyo.
Wachezaji hao mpaka sasa hatma yao haijajurikana kwenye klabu ya Arsenal, huku Lacazette mkataba wake ukiisha mwishoni mwa msimu huu, na Salib ambaye yupo kwa mkopo kwenye klabu ya Marseille.

“Nahisi ataondoka mwishoni mwa msimu kwa sababu ya matatizo aliyokuwa nayo na Arteta tangu msimu uliopita. Alisema William Gallas
‘Pindi Arteta alipochukua mikoba ya kuinoa klabu, Lacazette alikuwa kwenye kiwango kizuri, alikuwa anafunga magoli, anacheza mbele na Aubameyang pembeni. Lakini taratibu kukawa na matatizo na kocha, na Lacazette akawa hapati nafasi ya kucheza mechi nyingi.
“Ndio maana nadhani atahitaji kuondoka. Ni ngumu lwa mchezaji kama Lacazettekwa sababu kama mchezaji mkubwa, mara zote unataka kucheza mashindano makubwa.”
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.


