Mchezaji nyota wa klabu ya Chelsea Romelu Lukaku ambaye ameshindwa kuonyesha makali yake ambayo yaliwafanya viongozi wa klabu hiyo kukubali kulipa kiasi cha £100 million kuweza kumrudisha Uingereza anaweza kurudi alikotoka mwishoni mwa msimu.

Romelu Lukaku ambaye ameendelea kuwa na ukame wa kutofunga kwa muda mrefu kwenye michuano karibia yote ambayo maecheza hivi karibuni, ikiwemo michezo ya ligi kuu na klabu bingwa kwenye kalenda ya msimu huu.

Lukaku

Mapema mwaka huu Lukaku aliweka wazi hali yake ya kutokuwa na furaha kwenye klabu hiyo, ambapo mpaka sasa amefanikiwa kufunga magoli matano tu msimu huu, ambao unakwenda kuisha mwezi ujao.

Mchezaji huyo wa kimataifa ambaye alihigharimu kiasi cha £100 million Chelsea kutoka Inter Milan, ambapo huko alifanikiwa kufunga magoli 64, na kuisadia kuchukua ubingwa wa Serie A, anaweza kuwa njiani kurudi nchini Italia lakini sasa hivi atekwenda Ac Milan.

Kulingana na mtandao wa Goal, kwa sasa lukaku anathamani ya £77 million, ambayo ni ada kubwa kwa Ac Milan kuweza kulipa na mshahara wake ambao ni £325,000 kwa wiki, ikiwa atahitaji kuondoka London basi itabidili akubali kupunguza mshahara wake na chelsea wapunguze ada ya usajiri.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa