Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG Luis Campos ameonesha kufurahishwa na kiwango kinachooneshwa na beki mkongwe aliejiunga katika klabu hiyo akitokea klabu ya Real Madrid.
Ramos amekua akicheza kwa kiwango kizuri kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ufaransa siku za hivi karibuni kitu kilichomvutia mkurugenzi wa timu hiyo.
Akifanya mahojiano na kituo kimoja na alipoulizwa kuhusu kumpa mkataba mpya beki huyo nguli “Nafurahishwa na Ramos na kama ataendelea kucheza kwenye ubora huo basi itakua hakuna sababu ya kutokumuongezea mkataba Ramos”.
Campos aliendelea kusistiza “Ramos ana msimu mzuri sana pamoja na Messi itakua jambo zuri kuwaongezea wote”.
Beki huyo amekua akiandamwa na majeraha tangu ajiunge na miamba hiyo mwaka 2021 na kushindwa kucheza wakati mwingi lakini kwa msimu huu inaonekana majeruhi yamekaa mbali nae na kumfanya kucheza kwa kiwango bora sana mpaka sasa.
Pia mkurugenzi huyo anatamani kumuongezea mkataba staa wa klabu hiyo Lionel Messi ambaye mkataba unamaalizika hivi karibuni huku akiwa kwenye kiwango bora kabisa.