Hayawi hayawi hatimaye yametimia mbio za kuwania ubingwa wa EPL zilifika mwisho kwa michezo 10, timu 20 zilikuwa viwanjani kukamilisha mechi ya 38 wapo waliyokuwa wakipambana kuepuka kushuka daraja, wapo waliyokuwa wakipambania kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao kubwa zaidi ilikuwa Mechi ya Liver na Man City ambao walikuwa wakiwania ubingwa msimu wa 2021-22.

Liverpool na Manchester City walikuwa wamepishana kwa alama moja pekee ambapo ushindi kwa timu zote ndiyo ulikuwa unaamua ubingwa uende wapi. Liverpool walishinda 3-1 dhidi ya Wolves wakati Man City wao walishinda kwa 3-2 dhidi ya Aston Villa.

Ilionekana kana kwamba Manchester City walikuwa wamekwama baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 zikiwa zimesalia dakika 15 kipyenga cha mwisho kulia, mabao ya Matty Cash na Philippe Coutinho yaliweza kuwachanganya vyema mashabiki na benchi la City.

Lakini City waliweza kufanya kitu kisichoaminika kwa kufunga mabao matatu ndani ya dakika tano, mabao mawili kutoka kwa Ilkay Gundogan na Rodri, yaliitosha kuwapa Citizens taji la nne la Premier League ndani ya misimu mitano.

Ilimaanisha Liverpool, licha ya kuichabanga Wolves 3-1, kumaliza nafasi ya pili na kuuwa tuamaini la kushinda mataji manne msimu huu, baada ya kutwaa Kombe la Ligi na kombe la FA na kujiandaa kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa wiki ijayo.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa