Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr imelezwa atakuepo kwenye mchezo 16 bora utaokaowakutanisha na timu ya taifa ya Korea Kusini kesho jumatatu.
Taarifa za ndani kutoka kambi ya timu ya taifa ya Brazil zinaeleza mchezaji huyo atarudi kwenye timu hiyo baada ya kukosa michezo miwili kwenye hatua ya makundi kwasababu ya majeraha aliyoyapata katika mchezo wa wanza dhidi ya Serbia.
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Korea Kusini ameeleza Neymar atakua sehemu ya kikosi kuelekea mchezo wa kesho wa hatua ya 16 bora.
Staa huyo alionekana akifanya mazoezi na wenzake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil siku ya jana na hicho kilikua kiashiria tosha cha kuonesha staa huyo amerejea na atakua tayari kwa mchezo unaofuata katika hatua ya mtoano.
Baada ya Neymar kutangazwa kurejea katika mchezo wa kesho imeibua shangwe kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil duniani kote wakionesha kufurahishwa kwa kiwango kikubwa kurejea kwa staa huyo tegemezi wa timu hiyo.

