Simba Queens, JKT kufungua pazia la ligi kuu leo

PAZIA la Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho Jumanne kwa mchezo mmoja kuchezwa kwenye uwanja wa Bunju Complex baina ya Simba Queens na JKT Queens.

Wakati Simba Queens wakifungua pazia hilo, watani wao Yanga Princess watashuka dimbani kesho kutwa Desemba 7 kwenye uwanja wa Uhuru Dar, wakipambana na Fountain Gate Princess.

Simba Queens, JKT kufungua pazia la ligi kuu leo

Huku michezo mingine ikipigwa pia kati ya Baobab Queens ambao watacheza na Aman Queens kwenye uwanja wa Ilulu Lindi, Alliance Girls watakipiga na Ceasia Queens kwenye dimba la Nyamagana Mwanza.

Huku The Tigers Queens watacheza na Mkwawa Queens pale jijini Arusha na utakuwa ndiyo mchezo wa mwisho kwenye mzunguko wa kwanza.

Ikumbukwe Simba Queens ndiyo mabingwa watetezi wakitwaa taji hilo mara tatu mfululizo, watacheza na JKT Queens wenye mataji mawili na wakijaribu kutafuta kurejea kwenye ubora wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.