Klabu ya Simba Queens ilitarajia kutua alfajiri ya kesho Dar es salaam wakitokea Uturuki ambako waliunganisha ndege kutoka Morocco baada ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake kutamatika.

Simba walimaliza katika nafasi ya nne ya mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 na Mamelody Sundowns ambao walifungwa 4-0 na AS Far Rabat kwenye mechi ya fainali.

Simba Queens, Simba Queens Wanatua na Bonasi ya Kibabe, Meridianbet

Simba kwa kufanikiwa kufika kwenye hatua ya nusu fainali pekee walifanikiwa kukunja dola za Marekani 200,000 zaidi ya milioni 400 za Tanzania, Lakini pia wakiwa wana ahadi ya kulamba bonus kubwa kutoka kwa viongozi.

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez alisema kuwa bonus ya kihistoria wanakwenda kupewa wachezaji hao na benchi la ufundi baada ya kufanya makubwa na kufikia malengo ya kufika nusu fainali kama walivyopanga.

“Ukiachana na bonus ambayo CAF watawapa Simba Queens, kuna bonus nyingine kutoka kwa uongozi ambayo ni kubwa na ya kihistoria ambayo watapewa na itakuwa siri haitasemwa popote kama ulivyo utaratibu wa taasisi,” alisema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa