Klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro inataarifiwa iko mbioni kumalizana na mchezaji wake wa kigeni kutoka nchini Congo Deo Kanda.
Mtibwa Sugar ambayo haiko vibaya msimu huu kwenye ligi kuu ya NBC ambapo mpaka sasa wako nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 24, Klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa kuachana na wachezaji wa kigeni wenye mchango mdogo kwenye timu.
Klabu hiyo imepanga kuachana na Deo Kanda na sababu ikiwa ni kua mchezaji huyo ana mchango mdogo kwenye timu hiyo, Huku akiwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye timu hiyo yenye maskani yake mkoani Morogoro.
Klabu ya Mtibwa Sugar mabingwa zamani wa ligi kuu Tanzania Bara wako kwenye mchakato huo mzito wa kuwapunguza wachezaji wenye mchango mdogo huku wakipokea mishahara mikubwa, Ikumbukwe wiki kadhaa nyuma klabu hiyo iliachana na golikipa wake raia wa Kenya Farouk Shikalo.

