Rais wa klabu ya Fc Barcelona Joan Laporta amesema kua mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwasasa anacheza klabu ya PSG Lionel Messi ndio mchezaji bora wa muda wote.
Mchezaji Lionel Messi amefanikiwa kushinda taji la kombe la dunia siku ya jumapili wakiifunga timu ya taifa ya Ufaransa katika mchezo wa fainali, Taji pekee ambalo mchezaji huyo alikua amelibakisha kwenye maisha yake ya soka.
Kufuatia kushinda taji la kombe la dunia kwa mchezaji Lionel Messi kumeibua mijadala mbalimbali wengi wakihitimisha kwa kusema kua ndio mchezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea, Na Rais Laporta nae ameungana na wadau wengine akisema mchezaji huyo ndio mchezaji bora wa muda wote.
Rais huyo wakati akifanya mahojiano na waandishi amempongeza mchezaji huyo wa zamani wa klabu yake na kusema mchezaji huyo ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo na pia mapigo yake ya moyo yanadunda Barcelona.
Rais Laporta alipoulizwa kuhusu kumrudisha mchezaji huyo klabuni hapo “Ni mchezaji wa klabu ya PSG kwasasa, Lakini siku tutamrudisha Messi hapa” Kutokana na kauli ya Rais huyo inaonesha moja kwa moja klabu hiyo ina mpango wa kumrudisha mchezaji huyo ndani ya Barcelona siku moja.

