Klabu ya soka ya wanawake ya Simba Queens imepata suluhu dhidi ya timu ya soka ya wanawake ya Yanga Yanga Princess kwa goli moja kwa moja.
Katika mchezo uliokua mkali na wenye kasi ulibahatika kuisha kwa mabao mawili huku kila timu ikifanikiwa kupata goli moja katika mchezo huo. Huku Klabu ya Yanga Princess ikifanikiwa kupata bao la mapema kabla ya watani zao.
kipindi cha kwanza kwenye dimba la Benjamin Mkapa kilimalizika kwa klabu ya Yanga Princess ikiongoza kwa bao moja kwa bila, Hiyo ni baada ya kuchongwa kwa kona safi na kumaliziwa na kichwa kizuri na Wogu Success na kuwafanya wananchi kwenda mapumziko kifua mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku klabu ya Simba Queens ikihitaji kusawazisha bao kwa udi na uvumba, Mpaka pale dakika ya 57 mshambuliaji wa klabu hiyo Vivian Corazone alipopiga shuti kali kutoka nje ya 18 na kwenda moja kwa moja wavuni na kufanya matokeo yawe moja kwa moja.
Klabu zote mbili kwa maana ya Yanga Princess na Simba Queens ziliendelea kuhakikisha zinapata alama tatu huku kila upande ukifanya mashambulizi kwa wakati wake, Lakini mchezo huo uliisha kwa sare ya bao moja kwa moja.

