Simba Queens waanza na mguu mbaya

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa upande wa Wanawake na Mabingwa wa Cecafa 2022 Simba Queens wameanza na mguu mbaya kwenye ligi baada ya kujikuta wakichapwa kwa mabao 2-1 na JKT Queens kwenye mechi ya ufunguzi jana Jumanne.

Simba Queens waanza na mguu mbaya

Simba Queens walikuwa wa kwanza kupata ushindi kupitia kwa Opah Clement kwa mkwaju wa penalty, kisha JKT wakasawazisha kupitia kwa Fatuma Mustapha na bao la pili na la ushindi likifungwa na Eto Mlenzi.

Hata hivyo Simba Queens walifanikiwa kupata penalty dakika za mwisho kipindi cha pili, kwa bahati mbaya kiungo wa Kenya Aquino Corozone alikosa penalty hiyo baada ya kupaa juu ya lango.

Huo unakuwa ushindi wa kwanza kwa JKT Queens baada ya misimu miwili kupita na hiyo inakuwa mara ya pili Simba Queens wanapoteza kwenye uwanja wao wa nyumbani Bunju Complex na mara zote wakifungwa na JKT.

Kocha wa Simba Charles Lukula raia wa Uganda alitupa lawama kwa wachezaji wake kwa kushindwa kutimiza majukumu yao: “Tumepoteza mchezo wa kwanza jambo ambalo siyo nzuri kwetu sisi kama mabingwa watetezi.

Simba Queens waanza na mguu mbaya

“Nafikiri wachezaji wangu walishindwa kutimiza majukumu yao sawa sawa. Naomba radhi kwa mashabiki kwa kukosa furaha kwenye mchezo huu. Ahadi yetu ni kwamba tunakwenda kurekebisha kwenye mechi zijazo.”

Kwa upande wa kiungo wa JKT Queens Eto Mlenzi alisema: “Tiulikwenda kucheza na Simba Queens, tukiwa tunajua wao ni mabingwa watetezi na wamefanya vizuri kimataifa hivyo tulicheza kwa kuwaheshimu.”

leo kuna mechi zingine nne, ikiwemo kubwa ya Yanga Princess na Fountain Gate Princess inayochezwa uwanja wa Uhuru Dar.

 

Acha ujumbe