Rais wa shirikisho la mpira duniani Fifa Gianni Infantino amesifu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na kusema ni bora zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu.
Rais huyo anaamini kombe la dunia la mwaka huu kwenye hatua ya makundi limeonesha ubora mkubwa licha ya mapingamizi ambayo kombe hilo ilikumbana nayo wakati michuano hiyo inakaribia kuanza. Michuano hiyo iliyopigwa Qatar ilikumbwa na mapingamizi kwa kiwango kikubwa kutoka nchi za ulaya ambazo zilikua zinaunga mkono mapenzi ya jinisia moja.Rais Infantino anasema licha ya kombe la dunia kupata mapingamizi mengi mwaka huu lakini aliamini ubora wa timu uwanjani utaipa michuano hiyo ubora mkubwa na ndo kilichotokea mpaka sasa. Hakuna timu iliyofanikiwa kupata alama 9 kwenye hatua za makundi mwaka huu nchini Qatar.
Michuano hiyo pia imeshuhudia vigogo kama Ujerumani na Ubelgiji wakitokea hatua za makundi na hii inaonesha kwa namna michuano ya kombe la dunia msimu huu yamekua bora sana na ushindani mkubwa. Rais Infantino anasema hii hatua bora ya makundi kwenye michuano ya kombe la dunia ambayo haijawahi kutokea kwakua imeonesha hakuna tena timu ndogo wala kubwa kwenye michuano hiyo na timu zote zikishafika kwenye michuano zipo sawa.
Michuano ya kombe la dunia msimu huu ambapo imeshuhudia timu kutoka kila ikifanikiwa kufuzu hatua ya mtoano ikiwa ni mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la dunia na hii inajaribu kuonesha ni kwa namna mpira umekua katika kila eneo duniani.