Staa wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania Eden Hazard ametangaza rasmi kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Ubelgiji.

Hii imekuja siku chache baada ya timu ya taifa ya Ubelgiji kuondolewa kwenye michuano ya kombe la dunia inayopigwa nchini Qatar kwenye hatua ya makundi. Timu ya taif ya Ubelgiji ilimaliza nafasi ya tatu kwenye kundi F baada ya kukusanya alama nne tu na kufanya kuondolewa kwenye michuano hiyo.hazardKupitia mtandao wake wa kijamii Eden Hazard ameandika ujumbe mrefu ambao unadhihirisha kua hatakuepo tena kwenye timu ya taifa ya Ubelgiji na ni rasmi ameamua kufunga ukurasa huo na kuendelea kujikita zaidi kwenye klabu yake.

Hazard ambaye ameanza kuitumikia timu hiyo toka mwaka 2008 amewashukuru sana mashabiki wa nchi hiyo kwa upendo, ushirikiano, na kipindi chote cha furaha walichofurahia kwa pamoja wakati akitumikia taifa hilo kuanzia mwaka 2008 mpaka mwezi November 2022.hazardStaa huyo ameitumikia timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye michezo 126 huku akifunga jumla ya mabao 33 na kupiga pasi za mabao 36. Staa huyo aameamua kutoa mkono wa kwaheri kwa taifa hilo huku akikumbukwa zaidi kwa ubora aliounesha kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi ambapo walimaliza nafasi ya tatu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa