Eden Hazard anakubali kuwa Ubelgiji ilikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda Kombe la Dunia wakati ‘kizazi chao cha dhahabu’ kilikuwa katika kilele chake mnamo 2018.

Ubelgiji ilifurahia Kombe lao bora la Dunia miaka minne iliyopita nchini Urusi ilipomaliza ya tatu kufuatia kichapo cha 1-0 kutoka kwa washindi Ufaransa katika hatua ya nusu fainali.
Lakini baada ya kushindwa na Italia katika robo fainali ya Euro 2020, kuna dhana kwamba kizazi kikubwa cha wachezaji wa Ubelgiji kimekosa nafasi ya kushinda kombe kuu.
Ingawa kikosi chao nchini Qatar kinajumuisha majina mengi yanayofahamika na wanachama kadhaa wa ‘kizazi cha dhahabu’, inakubalika wengi wao wamepita kiwango chao bora, na ushindi wa 1-0 dhidi ya Canada haukusaidia sana kukanusha wazo hilo.

Hazard, ambaye ana umri wa 31 na amekuwa akikumbwa na majeraha akiwa Real Madrid katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ana uhalisia kuhusu nafasi za Ubelgiji, lakini alikuwa na nia ya kuwakumbusha wakosoaji kwamba timu ya Roberto Martinez bado ina mengi kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Hazard amesema kuwa; “Kusema haki, nadhani tulikuwa na nafasi nzuri zaidi miaka minne iliyopita aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mchezo wa pili wa Kundi F wa Ubelgiji dhidi ya Morocco, kwani timu ilikuwa bora miaka minne iliyopita lakini bado tuna ubora wa kushinda michezo.”
Hazard aliongeza kwa kusema kuwa wana vijana wachache ambao ni wakubwa kwasasa lakini wana uzoefu, wana kipa bora ambae ni Thibaut Courtois, pia wana moja ya viungo bora zaidi Duniani na washambuliaji wazuri pia.

Ubelgiji ilikosolewa vikali kwa uchezaji wao dhidi ya Canada, mwishoni mwa mchezo, Kanada ambao walipata penalti na Alphonso Davies akaikosa baada ya kuokolewa na Courtois.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


