Beki wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James amerejea rasmi kwenye kikosi cha Chelsea baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi aliyokua ameyapata.
Beki Reece James amekua nje ya uwanja tangu mwezi Oktoba ambapo alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Ac Milan, Beki huyo alipata majeraha ya goti na ndio yaliomueka nje ya uwanja.
Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza alikosa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar iliomalizika wiki kadhaa zilizopita kutokana na majeraha hayo aliyoyapata tangu mwezi Oktoba, Lakini beki huyo ameweza kurejea kwenye kikosi cha Chelsea.
Beki huyo amerejea kwenye kikosi cha Chelsea rasmi baada ya kutoka kwenye majeraha na hiyo imethibitika baada ya klabu ya Chelsea kutoa kikosi ambacho kitacheza dhidi ya klabu ya Afc Bournamouth, Ndipo jina la beki huyo lilipojitokeza.
Baada ya kurejea kwa Beki Reece James kutoka kwenye majeraha klabu ya Chelsea inaendelea kupunguza idadi ya majeruhi ambayo imekua nao, Kwani klabu ya Chelsea imeandamwa na majeraha kwa kiwango kikubwa sana.

