Reece James Arejea Kikosini

Beki wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James amerejea rasmi kwenye kikosi cha Chelsea baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi aliyokua ameyapata.

Beki Reece James amekua nje ya uwanja tangu mwezi Oktoba ambapo alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Ac Milan, Beki huyo alipata majeraha ya goti na ndio yaliomueka nje ya uwanja.reece jamesBeki huyo wa kimataifa wa Uingereza alikosa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar iliomalizika wiki kadhaa zilizopita kutokana na majeraha hayo aliyoyapata tangu mwezi Oktoba, Lakini beki huyo ameweza kurejea kwenye kikosi cha Chelsea.

Beki huyo amerejea kwenye kikosi cha Chelsea rasmi baada ya kutoka kwenye majeraha na hiyo imethibitika baada ya klabu ya Chelsea kutoa kikosi ambacho kitacheza dhidi ya klabu ya Afc Bournamouth, Ndipo jina la beki huyo lilipojitokeza.reece jamesBaada ya kurejea kwa Beki Reece James kutoka kwenye majeraha klabu ya Chelsea inaendelea kupunguza idadi ya majeruhi ambayo imekua nao, Kwani klabu ya Chelsea imeandamwa na majeraha kwa kiwango kikubwa sana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.