Usajili mpya kwenye dirisha dogo la usajili ndani ya klabu ya Simba Saidoo Ntibazonkiza ameanza na moto wa hatari ndani ya klabu ya Simba baada ya kufunga Hattrick leo dhidi ya Tanzania Prisons.
Kiungo huyo mshambuliaji katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons amefanikiwa kufunga mabao matatu, Huku akicheza kwenye ubora mkubwa na kuisaidia klabu yake ya Simba kushinda kwa jumla ya mabao saba kwa moja.
Saidoo Ntibazonkiza anaingia katika rekodi ya kua miongoni mwa wachezaji watatu pekee ambao wamefunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja msimu huu, Akiungana na nahodha wake John Bocco pamoja na Fiston Kalala Mayele.
Mchezaji huyo ambaye kwa mara ya kwanza anaitumikia klabu ya Simba amefanikiwa kucheza kwa ushirikiano kwa mkubw ana wachezaji wenzake kana kwamba alikua ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu, Lakini kumbe ndio mchezo wake wa kwanza.
Kiungo Ntibazonkiza sasa anafanikiwa kuhusika kwenye mabao 14 msimu baada ya kufunga mabao saba na kupiga pasi saba za mabao, Kabla ya mchezo wa leo kiungo huyo alikua amehusika kwenye mabao 10 akiwa na waajiri wake wa zamani Geita Gold lakini leo akifanikiwa kufunga mabao matatu na kutengeneza moja hivo kunamfanya kuhusika kwenye mabao 14.

