Simba Yafanya Kufuru kwa Mkapa Yaicharura Prisons Wiki

Klabu ya soka ya Simba imemaliza mwaka kwa aina yake baada ya kufanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao saba kwa moja dhidi ya klabu ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

Klabu ya Simba iluanza mchezo huo ikiwa na kasi wakionesha wana jambo lao mapema tu nahodha John Bocco akawapatia wenyeji bao la kuongoza kupitia pasi safi ya Saiddo Ntibazonkiza, na kuwafanya wekundu wa msimbazi kuongoza mchezo huo.

Baada ya wekundu wa Msimbazi kupata bao la kuongoza dakika chache zilizofuata mshambuliaji wa Prisons Samson Mbangula alifanya faulo ya hatari kwa beki wa Simba Henock Inonga, Kufuatia faulo hiyo Mbangula alikwenda nje kwa kadi nyekundu huku Inonga pia akishindwa kuendelea na mchezo baada ya rafu hiyo mbaya.simbaBaada ya Prisons kupata kadi nyekundu dakika chache mbele walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Jeremiah Juma, Hivo kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya goli moja kwa moja.

Kipindi cha pili Lunyasi walianza mchezo kama nyuki ikiwa ni dakika ya 46 tu ya mchezo mshambuliaji Bocco anawatanguliza wekundu wa msimbazi kwa mara nyingine, Kabla ya Sadio Ntibazonkiza kuweka kambani bao la tatu la mchezo.

Ingizo Jipya kwenye kikosi cha wekundu wa msimbazi alifanikiwa kufunga bao lake la pili la mchezo likiwa la nne kwa upande wa Simba,Na kuifanya klabu hiyo kuongoza kwa mabao manne kwa moja huku wakiendelea kutandaza soka safi.simbaNahodha John Bocco alifanikiwa kufunga bao la tatu kwenye mchezo huo dakika ya 62 na kufanya klabu hiyo kuongoza kwa mabao matano na kufanikiwa kupiga hattrick yake ya pili msimu huu, Lakini mchezaji Ntibazonkiza nae alifanikiwa kufunga bao lake la tatu kwenye mcheo huo dakika ya 63 ya mchezo na kuwafanya wekundu wa msimbazi kuongoza kwa mabao sita kwa moja.

Beki wa Kulia Shomari Kapombe ndio alikamilisha karamu ya mabao kwa leo baada ya kufunga bao la saba la mchezo dakika ya 88 ya mchezo huku likiwa bao lake la pili msimu huu kwenye ligi ya NBC, Klabu ya Simba inaufunga mwaka 2022 kwa aina yake baada ya kupata ushindi mnono wa mabao saba kwa moja dhidi ya Prisons.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.