Ntibazonkiza Ameanza na Moto Simba

Usajili mpya kwenye dirisha dogo la usajili ndani ya klabu ya Simba Saidoo Ntibazonkiza ameanza na moto wa hatari ndani ya klabu ya Simba  baada ya kufunga Hattrick leo dhidi ya Tanzania Prisons.

Kiungo huyo mshambuliaji katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons amefanikiwa kufunga mabao matatu, Huku akicheza kwenye ubora mkubwa na kuisaidia klabu yake ya Simba kushinda kwa jumla ya mabao saba kwa moja.ntibazonkizaSaidoo Ntibazonkiza anaingia katika rekodi ya kua miongoni mwa wachezaji watatu pekee ambao wamefunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja msimu huu, Akiungana na nahodha wake John Bocco pamoja na Fiston Kalala Mayele.

Mchezaji huyo ambaye kwa mara ya kwanza anaitumikia klabu ya Simba amefanikiwa kucheza kwa ushirikiano kwa mkubw ana wachezaji wenzake kana kwamba alikua ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu, Lakini kumbe ndio mchezo wake wa kwanza.ntibazonkizaKiungo Ntibazonkiza sasa anafanikiwa kuhusika kwenye mabao 14 msimu baada ya kufunga mabao saba na kupiga pasi saba za mabao, Kabla ya mchezo wa leo kiungo huyo alikua amehusika kwenye mabao 10 akiwa na waajiri wake wa zamani Geita Gold lakini leo akifanikiwa kufunga mabao matatu na kutengeneza moja hivo kunamfanya kuhusika kwenye mabao 14.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.