Vinicius Jr Ailaumu La liga Baada ya Kufanyiwa Ubaguzi

Mchezaji wa klabu ya Real Madrid raia wa Brazil Vinicius Jr ameitupia lawama bodi ya ligi nchini Hispania La liga baada ya kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Mchezaji huyo alifanyiwa vitendo vya ubaguzi katika mchezo wa ligi kuu nchini humo na mashabiki wa klabu ya Real Valladolid baada ya kufanyiwa mabadiliko, Mchezaji huyo alionekana kutupiwa chupa za maji kutoka kwa mashabiki huku wakimrushia maneno ya kibaguzi kwa nyota huyo.vinicius jrKatika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania ambapo Real Madrid walikaribishwa na klabu ya Real Valladolid huku Real Madrid wakishinda kwa mabao mawili kwa bila, Ndipo Vinicius Jr alipokumbana na vitendo vya kibaguzi kutoka kwa mashabiki hao.

Hii inakua sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na kumfanya kuwashukia mabosi wa ligi hiyo, Kwani yeye anaona hakuna hatua zozote wanazochukua dhidi ya ubaguzi wa rangi unaofanywa na mashabiki.vinicius jrKupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Vinicius Jr alionekana kuwatupia lawama viongozi wa ligi hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo hivyo, Mchezaji huyo ameandika “Wabaguzi wa rangi wanaendelea kwenda kwenye viwanja kutazama klabu kubwa duniani, Lakini hakuna kitu La liga inafanya,Nitaendelea kuinua kichwa changu nikishangilia ushindi wangu na ule wa Madrid”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.