Klabu ya Yanga inaelezwa imeachana na mpango wa kuwasajili wachezaji wawili wa klabu ya Azam James Akaminko na Kipre Junior sababu ikiwa dau kubwa.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC walipeleka barua kwa klabu ya Azam siku kadhaa zilizopita ya kuwahitaji wachezaji hao wawili, Lakini klabu hiyo imechana na mpango huo baada ya kutajiwa kiasi kikubwa cha pesa kwa kila mchezaji na klabu ya Azam.
Klabu ya Azam Fc inaelezwa wamehitaji dola laki nne kwa kila mchezaji ambaye Wananchi walimuhitaji dola laki nne kwa pesa za kitanzani ni sawa ni shiilingi milioni mia tisa kwa kila mchezaji, Hivo Yanga wameamua kuachana na mpango huo baada ya kushindwa kumudu gharama hizo.
Klabu ya Yanga walihitaji wachezaji hao wawili ili kuweza kukiimarisha kikosi chao kuelekea michuano ya kimataifa msimu huu, Pamoja na kutetea mataji ambayo walitwaa msimu uliomalizika kama ubingwa wa ligi kuu na pamoja na kombe la Azam.
Yanga pia walihitaji kuhakikisha wanaziba pengo la kiungo wao mahiri ambaye ameondoka klabuni hapo siku za hivi karibuni Feisal Salum, Na James akaminko alikua anaonekana anaweza kua mbadala sahihi wa kiungo huyo kutoka visiwani Zanzibar.

