La liga Wafungua Kesi Rasmi Kisa Vinicius Kubaguliwa

Shirikisho la soka nchini Hispania La liga limefungua kesi rasmi kwenye mahakama ya ndani nchini dhidi ya waliomfanyia ubaguzi mchezaji wa Real Madrid Vinicius Jr.

Mchezaji wa Real Madrid Vinicius Jr alifanyiwa ubaguzi katika mchezo dhidi ya Real Valladolid ambapo mashabiki wa timu ya Valladolid walimfanyia vitendo vya Ubaguzi mchezaji huyo. Vini alifanyiwa ubaguzi wakati amefanyiwa mabadiliko na kuanza kurushiwa chupa na kutupiwa maneno ya kibaguzi na mashabiki hao.la ligaLa liga wamewaadhibu mashabiki hao waliohusika kwenye kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya Vinicius ikiwa ni pamoja na kufungua mashtaka dhidi yao baada ya kufanya vitendo vya kibaguzi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Vinicius ambaye aliilaumu La liga baada ya kushindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya mashabiki ambao wamekua wakionesha ubaguzi hadharani kwenye viwanja vya michezo na kusema haoni hatua ikichukuliwa, Shirikisho hilo rasmi leo limechukua hatua dhidi ya wabaguzi hao.la ligaKutokana na kilichoendelea siku ya leo inaweza kutafsirika kua shirikisho hilo limesikia kilio cha mchezaji Vinicius Jr ambaye alililamikia shirikisho kwa kutochukua hatua zozote dhidi ya wabaguzi, Lakini pia inaweza kupunguza ubaguzi kutokana na adhabu kali ambayo itakwenda kuwakuta wabaguzi hao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.