Xavi Amuunga Mkono Depay Kusalia Klabuni Hapo

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amekiri kufurahishwa na mshambuliaji wake raia wa Uholanzi Memphis Depay baada ya kugoma kuondoka kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Memphis Depay amekua akihusishwa kuondoka klabuni hapo kwa muda mrefu ikiwa ni tangu dirisha kubwa la majira ya joto, Lakini mchezaji huyo ameamua kusalia klabuni hapo hata kipindi hichi cha majira ya baridi mwezi Januari.xaviKocha Xavi ameweka wazi kua anavutiwa na kikosi kilichopo kwasasa na anaamini kinaweza kufanya vizuri kwenye michuano iliyopo mbele yao, Hii ni kutokana na klabu hiyo kutokuingia sokoni mwezi Januari hivo kuondoka kwa mchezaji ingekua pigo kubwa kwao.

Mchezaji Memphis Depay ataendelea kusalia ndani ya klabu ya Fc Barcelona na kocha wa klabu hiyo Xavi anasema anafurahishwa na mchezaji huyo kuendelea kuwepo klabuni hapo, Na anatarajia mabadiliko kuelekea mzunguko huu wa pili wa ligi.xaviMemphis Depay licha ya kucheza michezo mitatu tu msimu huu ndani ya klabu ya Barcelona lakini ameamua kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Catalans, Mchezaji huyo amekua akihusishwa na kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Manchester United lakini imekua tofauti kutokana na uamuzi wake wa kuendelea kusalia ndania ya Barcelona.

Acha ujumbe