Klabu ya Fc Bayern Munich imefanikiwa kumsajili golikipa kutoka klabu ya Borussia Monchengladbach Yann sommer inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani katika dirisha dogo la mwezi Januari.
Klabu ya Bayern Munich imeweza kulipa kiasi cha euro milioni nane kwenda kwa klabu ya Borussia Monchengladbach ili kweza kumnasa golikipa wa kimataifa wa Uswisi Yann Sommer. Mabingwa hao wa Ujerumani walikua wakitafuta golikipa sokoni kipindi hichi cha mwezi Januari.
Bayern Munich walihitaji golikipa mzuri sokoni baada ya golikipa wake namba moja Manuel Neuer ambaye amefanyiwa upasuaji hivo kukosekana msimu wote uliobakia, Klabu hiyo iliamua kutafuta mbadala sahihi wa golikipa huyo na kwasasa imefanikiwa.
Yann Sommer ni golikipa mzuri mwenye ubora mkubwa ambaye amekua amejitengenezea sifa katika ligi kuu ya Ujerumani, Rasmi amejiunga na mabingwa wa Ujerumani akienda kuchukua nafasi ya Manuel Neuer aliyepata majeraha.
Golikipa huyo atakwenda ndani ya klabu ya Bayern Munich kushirikiana na golikipa namba mbili wa timu hiyo Sven Ulreich. Taarifa zinaeleza Yann Sommer anakwenda kua Golikipa namba moja ndani ya timu hiyo kwa kipindi hichi.

