Kiungo wa klabu ya soka ya As Roma ya nchini Italia Nicolo Zaniolo anatarajiwa kubakia ndani ya klabu hiyo baada ya kutaka kuondoka klabuni hapo hapo mwanzo.
Kocha Jose Mourinho ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari leo kua mchezaji huyo atasalia ndani ya klabu ya As Roma baada ya kuripotiwa mwanzo kutoka kuondoka, Zaniolo aliripotiwa kulazimisha kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha hili dogo la mwezi Januari.
Kiungo Nicolo Zaniolo alitaka kuondoka klabuni hapo ndani ya mwezi Januari mwaka huu kama ambavyo ameeleza kocha Jose Mourinho, Kiungo huyo alikaribia kujiunga na klabu ya soka ya Bournamouth inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ungereza lakini dili hilo lilikufa mwishoni na kumfanya kiungo huyo kusalia ndani ya Roma.
Klabu ya Tottenham ambayo ilionekana kuhitaji saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Italia lakini baada ya klabu ya Tottenham kufanya usajili wa winga kutoka Villarreal Arnaut Danjuma, Basi ikaonekana mpango wa kumsajili Zaniolo umekufa na ndipo Bournamouth walipoingilia dili na kiungo huyo hakuvutiw na ofa yao na kuamua kusalia As Roma.
Kocha Jose Mourinho amethibitisha kua mchezaji huyo aliomba kuondoka ndani ya klabu hiyo wiki kadhaa nyuma na yeye alimruhusu kwani hakua tayari kubaki na mchezaji ambaye hayupo tayari kuipambania klabu, Lakini baada ya dili lake kufeli basi mchezaji huyo atasalia ndani ya viunga vya Estadio de Olympico.

