Mourinho Aipongeza Napoli

Kocha wa klabu ya As Roma Jose Mourinho ameipongeza klabu ya Napoli chini ya kocha Luciano Spalletti kua wanaonekana tayari wanaweza kua mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Italia Serie A.

Klabu ya Napoli mpaka sasa inaongoza ligi kuu ya soka nchini Italia ikiwa na alama 12 mbele ya mabingwa watetezi Ac Milan ambao wanakamata nafasi ya pili, Klabu ya Napoli mpaka sasa imefanikiwa kushinda michezo 16 kati ya 19 iliyocheza na kupoteza mchezo mmoja pekee.MourinhoNapoli inakua timu ya tatu kushinda michezo 16 katika ligi kuu ya Italia baada ya Juventus kufanya hivyo mara tatu, Inter Milan mara moja kutokana na hali hii ndio inafanya kocha wa klabu ya As Roma Jose Mourinho kuamini inawezekana kabisa klabu ya Napoli ndio wanaenda kua mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka nchini Italia.

Klabu ya As Roma kesho watakua ugenini kumenyana na vinara hao wa ligi kuu ya Italia Napoli katika dimba la Armando Maradona, Na kocha Jose Mourinho lengo lake kubwa anasema ni kupata alama katika mchezo huo bila kujali kama tayari wametwaa ubingwa ubingwa.MourinhoMchezo kati ya Napoli na As Roma ni mchezo unaotarajiwa kua mkali na wa kusisimua kwani klabu ya Napoli wakiwa nyumbani watahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kujisimika kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Italia na kusafisha njia ya kwenda kua mabingwa, Lakini As Roma wao watakua wanatafuta alama tatu ili kutafuta nafasi ya kwenda kucheza michuano ya ligi ya mabingwa ulay msimu ujao.

Acha ujumbe