Real Madrid Inachechemea La liga

Klabu ya soka ya Real Madrid imeendelea kuchechemea katika ligi kuu nchini Hispania baada ya kukubali kichapo cha goli moja kwa bila dhidi ya klabu ya Real Mallorca.

Real Madrid wakiwa ugenini wamekubali kipigo cha goli moja kwa bila hii ikimaanisha wanaendelea kuongeza pengo la alama baina yao na vinara wa ligi hiyo klabu ya Barcelona. Mabingwa hao watetezi wameacha kwa alama tano na klabu ya Barcelona ambao hawajacheza mchezo wao dhidi ya Sevilla usiku wa leo.Real MadridVijana wa Carlo Ancelotti wamekua hawana muendelezo bora toka warudi kutoka kwenye michuano ya kombe la dunia kwani wameshafungwa michezo mitatu kwenye michuano yote huku wakipoteza miwili kwenye ligi kuu ya Hispania, Hii inaonesha namna ambavyo wapo kwenye wakati mgumu.

Real Madrid kwenye michezo yao kumi ya mwisho wameshinda mitano na kufungwa mitatu huku wakisuluhu michezo miwili, Hii inawaeka kwenye wakati mgumu zaidi kuelekea kwenye mbio za kutetea taji lao ndani ya msimu huu.Real MadridKlabu ya Fc Barcelona kama watafanikiwa kushinda mchezo wao wa leo dhidi ya klabu ya Sevilla usiku wa leo basi wataiacha klabu ya Real Madrid kwa jumla ya alama nane, Mabingwa hao watetezi watakua na mlima mrefu wa kuupanda ili kutetea taji lao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.