Klabu ya Manchester City inakwenda kwenye uwanja wa Totteham Hotspurs leo ikiwa na rekodi mbaya kwani haijawahi kushinda mchezo wowote katika uwanja huo tangu mwaka 2019.
Kwa kipindi cha hivi karibuni Manchester City wamekua wakipata tatu wanapokutana na klabu ya Tottenaham Hotspurs kabla ya kufanikiwa kushinda mchezo wa mwisho walipokutana, Lakini bado njozi mbaya zinaweza kuwaandama vijana wa Pep Guardiola leo watakapocheza mchezo wao dhidi ya vijana wa Antonio Conte wakiwa ugenini.
Klabu ya Tottenham mara ya mwisho walipokutana na Man City katika dimba la Etihad walifungwa kwa jumla ya mabao manne kwa mawili, Huku vijana wa Guardiola wakitoka nyuma kwa mabao mawili waliyotanguliwa na kushinda mchezo huo.
Manchester City wamefungwa katika michezo yote minne ya mwisho waliyocheza na klabu ya Tottenham ikiwa nyumbani kwao tangu mwaka 2019, Lakini pia sio kufungwa tu Man City hawajafanikiwa kupata goli hata moja katika michezo hiyo jambo ambalo linaweza kuwapa presha katika mchezo wa leo.
Klabu ya Manchester City wanaenda kucheza na Tottenham wakijua kabisa huu ni mchezo muhimu zaidi kwao ya kuweka matumaini hai katika mbio zao za kutetea taji la ligi kuu ya Uingereza, City wako nyuma kwa alama tano dhidi ya vinara Arsenal hivo wakifanikiwa kushinda mchezo wa leo watapunguza pengo la alama mpaka kufikia mbili baada ya Arsena kupoteza mchezo jana dhidi ya Everton.

