Sancho Afurahi Kufunga Tena Ndani ya United

Winga wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Jadon Sancho amefurahi kufunga bao tena ndani ya kikosi hicho baada ya kukosekana kwa zaidi ya miezi mitano ndani ya timu hiyo.

Winga Jadon Sancho amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu akiwa anasumbuliwa na majeraha pamoja na saikolojia yake haikua vizuri kama ambavyo kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag aliwahi kueleza miezi kadhaa nyuma.SanchoWinga huyo huyo amefanikiwa kufunga bao jana katika mchezo wake wa pili tangu arejee klabuni hapo baada ya kukosekana tangu mwezi Oktoba mwaka jana, Jana mchezaji huyo alifunga bao la kusawazisha baada ya klabu yake kutanguliwa kwa mabao mawili na klabu ya Leeds United katika mchezo uliomalizika kwa mabao mawili kwa mawili.

Mchezaji huyo aliandika kupitia mitandao yake ya kijamii na kusema “Siwezi kukuambia kwa namna gani nilikosa hisia kama hii, Timu imeonesha sifa nzuri kubaki kwenye mchezo, Tutaenda tena wikiendi”SanchoBaada ya Jadon Sancho kufanya vizuri katika mchezo wa jana amemfanya kocha wa klabu hiyo kumpongeza mchezaji huyo kutokana na ubora ambao ameuonesha katika mchezo wa jana, Hiyo inaweza kumpa nguvu mchezaji na kuweza kumrejesha kwenye ubora wake ambao amekua nao tangu akiwa klabu ya Borussia Dortmund.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.