Ancelotti, Guardiola, Scaloni Kuwania Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka

Carlo Ancelotti, Pep Guardiola, na Lionel Scaloni wameingia kwenye tatu bora ya makocha ambao wanawania tuzo ya kocha bora wa mwaka 2022 kupitia shirikisho la soka duniani FIFA.

Kocha Carlo Ancelotti anaingia kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na makubwa ambayo aliyafanya na klabu ya Real Madrid kwa mwaka 2022, Kocha huyo aliiwezesha klabu yake kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya, kombe la ligi kuu nchini Hispania La liga, pamoja na kombe la Spanish Super Cup.AncelottiKocha Pep Guardiola yeye amekua kwenye kiwango bora sana msimu uliomalizika baada ya kuisaidia kubeba taji la ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya pili mfululizo, Huku akiisaidia klabu hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ni wazi kocha huyo anastahili kuwepo kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kocha Lionel Scaloni amekua kwenye kiwango bora sana akiiongoza timu ya taifa ya Argentina kuweza kunyakua taji la kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022 baada ya kupita  miaka takribani miaka 36, Hivo kocha huyo anaonekana kustahili kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho mpaka sasa.AncelottiMakocha Carlo Ancelotti, Pep Guardiola, pamoja na Lionel Scaloni wote wamefanya kazi kubwa wakiwa na timu zao, Na wanastahili kabisa kuwepo kwenye hatua hiyo waliyofika mpaka sasa lakini maamuzi yanasubiriwa ili kujua ni nani kati yao ataweza kunyakua tuzo hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.