Geita Gold Anaongoza 2-1 Dhidi ya Ruvu Mapumziko

Ligi kuu ya Tanzania Bara inaendelea hivi sasa kwa mchezo mmoja kati ya Geita Gold ya Geita dhidi ya Ruvu Shooting ambapo mwenyeji anaongoza mabao 2-1 mapumziko.

 

Geita Gold Anaongoza 2-1 Dhidi ya Ruvu Mapumziko

Mabao hayo kwa upande wa Geita yametupiwa kimyani na Sayte pamoja na Manyasi wakati kwa upande wa Ruvu bao limefungwa na Abrahamani dakika ya 44 kabla ya mapumziko.

Baada ya kuongoza mpaka sasa kipindi cha kwanza Vijana wa Fred Delix Minziro wamepanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wakijikusanyia pointi zao 34 hadi sasa kwenye ligi kuu ya NBC.

Ruvu wao wameendelea kushikilia nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kuwa wameshafungwa mpaka kufikia mapumziko na endapo wakifungwa hii leo hali yao itazidi kuwa mbaya.

Geita Gold Anaongoza 2-1 Dhidi ya Ruvu Mapumziko

Mpira ni dakika 90 na hapo bado 45 zingine. Je watafanya nini vijana hawa wa mBwana Makata kwenye dakika zilizosalia. Je Wachimba madini nao watakubali kunyanga’nywa uongozi wao?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.