Ligi kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa mchezo mmoja ambapo Geita Gold watakuwa nyumbani kukiwasha dhidi ya Ruvu Shooting ambao bado wanajitafuta kwenye ligi.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni katika Dimba la Nyankumbu huku kila timu ikihitaji pointi tatu muhimu ili iweze kusogea katika nafasi inayofuata kwenye msimamo.
Geita Gold yupo nafasi ya tano baada ya kucheza michezo yao 22, wakiw awameshinda mechi zao saba, sare kumi na kupoteza mara tano wakikusanya pointi zao 31 huku mechi ya mwisho wakishinda.
Wakati kwa upande wa Ruvu Shooting wao wakiwa nafasi ya 15 ambayo ni ya pili kutoka mwisho huku wakiwa wamekusanya pointi zao 17 wakiwa wameshinda mechi nne, sare tano na kupoteza mechi 13.

Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, Wachimba Dhahabu kutoka Geita waliondoka na ushindi. Je Ruvu wanaweza pata chochote kitu ugenini? Tembelea Meridianbet ubashiri michezo mbalimbali kwa ODDS KUBWA na za kibabe, pia kuna kasini ya mitandaoni kama Roulette, Poker, Sloti na Aviator.

