Klabu ya Fc Barcelona imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya klabu ya Valencia wakiwa katika dimba lao la nyumbani Camp Nou katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania La liga.
Barcelona wanapata ushindi leo baada ya kutoka kupoteza michezo miwili mfululizo ikiwemo kutupwa nje ya kombe la Europe league dhidi ya klabu ya Manchester United, Vilevile wakipoteza mchezo wa ligi kuu nchini humo wikiendi iliyopita dhidi ya klabu ya Almeria.
Bao la mapema la winga wa kimataifa wa Brazil Raphinha lilisaidia kuwapa alama tatu Blaugrana katika mchezo mgumu uliopigwa katika dimba la Camp Nou, Vinara hao wa ligi kuu nchini Hispania La liga walifanikiwa kulinda bao lao mpaka dakika 90 zinamalizika na kuibuka na na alama zote tatu.
Klabu ya Barcelona ingewezekana kupata mabao zaidi au kushinda zaidi ya goli moja lakini klabu hiyo ililazimika kucheza pungufu kuanzia dakika ya 59 mpaka dakika ya 90 ya mchezo, Kwani beki wake Ronald Araujo alioneshwa kadi nyekundu na kumaliza mchezo wakiwa pungufu.
Barcelona baada ya kushinda dhidi ya klabu ya Valencia katika mchezo wa leo wamefanikiwa kufikisha alama 62 na kuongoza kwa alama 10 juu dhidi ya wapinzani wake klabu ya Real Madrid, Lakini klabu ya Real Madrid itacheza mchezo dhidi ya Real Betis usiku huu hivo wakifanikiwa kushinda watapunguza pengo la alama mpaka kufikia 7.

